Teknolojia inakua kwa kasi sana. Takwimu zinaonesha kuwa watumiaji wa simu (hususa Android) wamekuwa wengi na wataongezeka kadri siku zinavyozidi kusogea. Hivyo ni vema kuchukua taarifa hizo kama fursa iliyo wazi kwa kila mmoja mwenye ndoto au wazo la kufikia watu wengi.
Taarifa nyingine nzuri ni kuwa mfumo wa android ndio rahisi zaidi kutengeneza apps zake, aidha uwe na ujuzi au usiwe nao kabisa. Kama ungependa kujua jinsi ya kutengeneza app ya android bila kuwa na ujuzi yani programming endelea kusoma post hii. Kama ungependa kujua namna ya kutengeneza app hizo kwa njia ya programming yani Android Studio na nyingine post hii haielezei kuhusu hilo japo unaweza kujifunza mambo kadhaa ambayo ni muhimu pia.
Hatua za kufuata kutengeneza app yako
1.Research (fanya uchunguzi)
Unatengeneza app kwa nini? Labda unataka kutatua tatizo fulani mfano app ya Thl ni utatuzi wa tatizo la notes kwa wanafunzi. Pia unaweza kuamua kutengeneza app kwa ajili ya burudani, app kwa ajili ya wewe kujifunza tu au hata app isiyokuwa na maana yoyote
Kama unatengeneza app kwa ajili ya biashara ni vizuri ukajua watumiaji watakuwa wa kina nani? watakuwa tayari kulipia? Unatoa huduma ambayo watu wataihitaji? na mengine yanayofanana na hayo
2.Tengeneza app yako
Ukishajua app unayohitaji kuitengeneza unakuja kwenye hatua muhimu kabisa ya kuitengeneza app yako. Njia rahisi ni kwa kutengeneza app online yaani katika website zinazotoa huduma hiyo. Unaweza kutumia njia hizi rahisi.
Web 2 Apk
Kama unataka kutengeneza app simpo tu kwa ajili ya blog au website yako ili ni chaguo bora. Unachotakiwa kufanya ni kuingia katika website yao unaweka website yako na baada ya sekunde kadhaa app yako inakuwa tayari. Hapa hakuna kujiunga ila ni lazima uwe na blog au website kwa ajili ya kutengeneza app yake.
Update : Web2Apk wamebadilisha huduma yao ya bure kuwa ya kulipia, hivyo kwa sasa kutumia huduma yao(iliyotajwa hapo juu) lazima ulipie kwanza
Andromo
andromo
Unataka kutengeneza app kwa ajili ya Masomo, sauti, ramani, picha, ukurasa wa youtube, blog au website unaweza tumia hii. Unachotakiwa kufanya ni kuingia katika website yao ili kuanza kutengeneza app yako. TanzaniaTech wameeleza hatua jinsi ya kutengeneza app kwa kutumia Andromo hapa
Website nyingine zinazoweza kufanikisha lengo lako ni kama
Appy Pie
AppMachine
Mobile Roadie
BiznessApps
BuzzTouch
TheAppBuilder
Good Barber
Kinetise
Como
DIY
App makr
AppsGeyser
Jmango
BuildFire
3.Test app yako
Hii ndiyo hatua inayofurahisha zaidi. Hapa unajaribu app uliyoitengeneza kama inakidhi vigezo na matarajio uliyoyaweka kabla ya kuitengeneza app yenyewe. Kama unatumia kompyuta kutengeneza ni vyema ukawa na simu kwa ajili ya ku test.
4.Sambaza app yako
Kama umemaliza ?hatua zote sasa unaweza kuiweka app yako katika platforms mbalimbali na hata kufanya matangazo kwa ajili ya kupata watumiaji. Unaweza kuiweka Google Play Store (ni muhimu kwa sababu watumiaji wengi wapo hapa), Amazon App Store na nyingine.
5.Zaidi
Nitanufaika vipi na kuwa na app?
Ukitengeneza app itakayotumiwa na watu wengi unaweza ingiza kipato kwa kuweka matangazo, kuifanya app ya kulipia (kabla mtu hajadownload) au kuuza vitu au huduma katika app yako.
Nawezaje kuiweka app yangu playstore?
Kuweka app playstore unatakiwa kufungua akaunti playstore ambayo inagharimu kiasi cha pesa kinacholipwa mara moja wakati wa kujiunga 25$ – kama Tsh 60,000.
Unahitaji kifaa gani simu au kompyuta?
Njia bora ni kwa kutumia kompyuta, lakini inawezekana kwa asilimia 100 kutengeneza kwa kutumia simu.
Ni vitu gani vingine vinahitajika?
kwa hatua tajwa hapo juu unahitajika uwe na kifaa chako (simu au kompyuta) na mb za internet angalau MB 500
Nitatumia muda gani kutengeneza hiyo app ?
Muda utategemea na uzoefu wako na utayari wa mahitaji yako kabla ya kutengeneza.
Endelea kutufuatilia ili kujua jinsi ya kutengeneza website na kujipatia kipato
27 Comments
Naitwa John Damiano nipo Daresalamu Ubungo nahitaji mwalimu wa kuweza kunifundisha kutengeneza App Ada nitalipia namba tangu 0768763701/0747151762
ReplyDeleteFind me
Deletesamahan kwa kuchelewa kujibu, ina naomba unitafte kwa 0626653295
Delete0763366610 nataka mtu anifungulie app ya kampuni tuiweke playstore
ReplyDeletesamahan kwa kuchelewa kujibu, ina naomba unitafte kwa 0626653295
DeleteAsante sana
ReplyDeleteNataka mtu anifundishe jinsi ya kutengeneza application 0620661412
ReplyDeletesamahan kwa kuchelewa kujibu, ina naomba unitafte kwa 0626653295
DeleteHellow kwa yeyote anaekua na swali awe ananitafuta kupitia e-mail blmcompany20@gmail.com au mathewchaburuma20@gmail.com pia number za simu ni 0626653295(ni vzuri ukanichek kupitia whatsapp)
ReplyDeleteAsanten sana wafuatiliaji wa blog hii pia naomba msamaha kwa kutojibu kwa haraka zaidi comments zenu kutokana na majukumu.
Mi hapa nilikuwa na swali ety kwamba jinsi ya kutengeneza app ya kuhifathia pesa
DeleteNatafuta mtu wakunifunza njisi yakufungua app please brother
ReplyDeleteboss number 0626653295
DeleteNahitaji mtu anifundishe kutengeneza app 0623231026
ReplyDeletenimekutumia message kwenye number yako
Deletenahitaji
ReplyDeletepiga simu number 0626653295
DeleteSBB.com.Helow bro,nahitaj kufungua app, nahitaji msaada wako
ReplyDeletecall us 0626653295
DeleteSBB.com.Helow bro,nahitaj kufungua app, nahitaji msaada wako
ReplyDeleteMahitaji fundi wa app
ReplyDeletecall us 0626653295
DeleteNahitaji mtu wakunifungulia app ya biashara naomba nipate jibu kwa mail yangu Mariamhemed42@gmail.com
ReplyDeleteNataka kujifunza kufungua application ya kuhifadhi nyimbo mtandaoni na kulipiwa kujipatia kipato 0655042621
ReplyDeleteHi ngumu
ReplyDeletehellow boss sio ngumu kama unavyofikiri
DeleteSorry bro, Je hicho kipato/malipo nayapataje nikiweka app yangu play store?
ReplyDeleteHupatikani kaka
ReplyDelete