Advertisment

Jinsi ya kutengeneza pesa kupitia smartphone yako

Karibu mpendwa msomaji.
Kwanza kabisa ningependa kutumia post hii kuomba radhi kwani nimekuwa kimya kwa muda mrefu sana. Lakini hii imekuwa ni kwa sababu ya masomo. Bado nipo shule hivyo inakuwa ngumu kufanya masomo, blogu na kazi. Nimejitahidi kujipangilia sana lakini mara nyingi ninapokuwa na muda huru huutumia kutengeneza kazi za wateja wangu na kujikuta nikiiacha blogu hii pembeni kidogo. Samahani na endelea kuwa nami.


Jinsi ya kutengeneza pesa ukiwa na smartphone?
Ni dhahiri kwamba hivi sasa idadi kubwa ya watu tayari wanamiliki smartphones. Smartphone ikiwa inamaanisha simu ambayo imeundwa kwa kuongezewa uwezo na kuweza kufanya idadi kubwa ya mambo ambayo hufanywa na computer, huweza kutumika kufanya mambo mbalimbali ambayo yatakusaidia wewe katika masuala yako ya kijamii na kiuchumi pia.

Leo nitaangalia kwa ufupi ni kwa jinsi gani unaweza kutumia smartphone kujipatia au kuboresha kipato chako kwa njia halali, (...wengine hutumia simu kuiba pesa za watu!)

> Hukusaidia kupata ramani ya mahali fulani (Kwa GPS)
Hivi pia inawasaidia wateja wako ambao wana ramani ya mji au mahali husika katika simu zao kuweza kukufikia kiurahisi. Lakini vilevile hata kama upo katika mji wa kigeni kwa shughuli zako za kibiashara,
smartphone yako ni rafiki mwema kwa hukusaidia kufika uendako kwa wakati muafaka.


> Unaweza kufuatilia habari za wateja.
Kupitia applications mbalimbali unaweza kuwa karibu na wateja (kwa biashara kubwa na ndogo). Unaweza kuwa na data zao katika simu yako. Kwa biashara kubwa jambo hili ni la muhimu sana kwani unapomuelewa zaidi mteja hukusaidia wewe kumtimizia kile anachohitaji.

> Uza Internet
Ndiyo. Ifanye smartphone yako kuwa internet cafe kwa kutumia wi-fi. Unaweza kugawa internet kwa watu waliokuzunguka na kisha wakakupatia pesa. Cha msingi ni kutafuta sehemu ambayo watu baadhi wanahitaji
mtandao na hawana modem au vifurushi. Ifanye smartphone yako iwe hotspot, hakikisha unatumia apps za kiusalama ili kuzuia watu kukuibia bando lako bila wewe kujua.


> Wasiliana na tunza akaunti zako katika kurasa za kijamii
Kwa kutumia mitandao ya kijamii utakuza zaidi biashara yako. Tumia smartphone yako ku update kurasa zako katika mitandao kama facebook, twitter na kadhalika.

> Piga picha.
Sio kila simu huweza kupiga picha nzuri. Lakini kama una smartphone original yenye uwezo mkubwa wa kupiga picha. Tumia simu yako kama kamera na unaweza kuwapiga watu na ukalipwa.


Shukrani kwa kusoma kipengele hiki, sababu hizi ni chache kati ya nyingi nilizokuandalia. Usikose kusoma Sehemu ya pili hapo baadaye kidogo. Kwa sasa, asante na endelea kuwa nami.

Smartphone ziko za aina nyingi tofauti. Zinabeba programu za muhimu sana zinazoweza kukusaidia katika biashara pia kujipatia kipato.
Asante kwa kusoma na naamin utayafanyia kazi

Post a Comment

0 Comments